🌿 TAURUS ♉️ • VIRGO ♍️ • CAPRICORN ♑️🔮 UJUMBE WA EARTH SIGNS “RESET”
🌿Mpenzi, ujumbe huu unaonyesha kwamba umekuwa ukibeba vitu vingi sana kiakili, kihisia, kiroho, na hata kifedha.
Umejaribu kuwa mtu mwenye nguvu, anayewajibika, anayeaminika na anayeshikilia kila kitu pamoja.
Lakini ujumbe wa Spirit ni: kwa nini bado unabeba mzigo ambao haukupaswa kuwa wako peke yako?🧠 Kwanza: Uchovu wa akiliBaadhi yenu akili imechoka sana. Unawaza mambo yaliyokwenda vibaya, mambo yanayopaswa kufanyika, na yale ambayo yanaweza kwenda vibaya baadaye.Unaweza kujikuta:ukiwa na mawazo mengi,ukirudia-rudia mambo kichwani,umechoka lakini akili haikubali kutulia,kuwa sensitive au emotional kuliko kawaida.Ujumbe ni pumzisha akili yako pia, si mwili pekee.
🌸 Pili: Anza kupokea, si ku-survive tuNishati inaanza kubadilika kuelekea comfort, uzuri, furaha na kujitunza.Hujaja duniani kwa ajili ya kulipa bills, kutatua matatizo na kuwajibika kila dakika.
😂Ujumbe mkubwa hapa ni:Usiweke furaha yako kama zawadi utakayopewa baada ya kuteseka. Tengeneza nafasi ya furaha sasa.Panga muda wa kupumzika kama unavyopanga muda wa kazi na majukumu.
👑 Queen of Cups — hisia zako si udhaifuKuna nguvu ya feminine energy inayojitokeza hapa.
Si lazima iwe kuhusu mwanamke; ni kuhusu kupokea, kujihudumia, kuheshimu hisia zako na kujiruhusu kupumzika.Unaweza kulia na bado ukawa na nguvu.Unaweza kuchoka na bado ukawa powerful.Unaweza kuhitaji msaada na bado ukawa na uwezo.Hupotezi taji lako kwa sababu umeamua kupumzika.
👑🔥 Na baada ya hapo… nguvu inarudiKuna energy mpya inayokuja motisha, ideas, confidence na drive vinaanza kurudi.Baada ya kipindi hiki kizito, unaweza kuanza kuhisi tena hamu ya kufanya mambo, kupanga maisha yako na kusonga mbele.
Lakini kuna tahadhari moja muhimu:Usirudi kwenye burnout mara tu unapopata nguvu.
Jifunze kutumia nguvu zako kwa hekima.
🌿 Ujumbe wa mwisho kwa Taurus, Virgo & Capricorn✨ Acha kuona kupumzika kama uvivu.
✨ Acha kubeba maumivu kama ushahidi kwamba wewe ni strong.
✨ Ruhusu furaha, softness na emotional release.
✨ Kubali pia kuhudumiwa na kusaidiwa.
✨ Usione aibu kulia, kusimama kidogo na kujipanga upya.Unaweza kupumzika na bado ukatawala maisha yako.
👑🌿🔑 Neno la ujumbe huu:RESET.Si lazima uanze upya maisha yako yote.
Wakati mwingine unahitaji tu kusimama, kuachilia mzigo usio wako, kupumua, na kurudi kwako mwenyewe. 💚