Leo nataka niwafunze kuomba uponyaji kwa elimu ya siri kutumia malaika Raphael, Raphael si mtu ,Raphael si binadamu wa kawaida; katika mapokeo ya dini na esoteric, anaelezwa kuwa Malaika Mkuu (Archangel)—kiumbe wa kiroho anayehusishwa na uponyaji, ulinzi na mawasiliano.
Fikiria Raphael kama Nguvu kuu iliopo katika Astral Realms na huwakilishwa na mwanga wa kijani basi fanya maombi haya kwa imani kwa siku tatu mfululizo utashare mrejesho hapa, kumbuka elimu hii si ya dini yoyote na mara nyingi natumia vitabu vya dini kama vessels zilizobeba sheria za ulimwengu.
MIZUNGUKO KWA AFYA NJEMATamka chant au mantra kwa sauti huku ukivuta pumzi taratibu na kwa mpangilio.
Rudia maneno haya kwa muda wa dakika 3–5 ili kuweka nia yako kwa nguvu.Unapozungumza, jione wewe mwenyewe, au sehemu yoyote ya mwili wako inayohitaji kutunzwa, ikiwa imezungukwa na mwanga mkali wa kijani wa zumaridi.
Huu unaelezwa kuwa ni mwanga wa Malaika Mkuu Raphael, anayehusishwa na uponyaji, ukirejesha mwili katika hali ya usawa na nguvu.
CHANT
Mwili wangu una nguvu, akili yangu iko wazi,Afya ndiyo ninayoitafuta na kuipata.Pumzi yangu ni ya kina, maisha yangu yana mwanga,Nimejazwa na mwanga wa uponyaji.
MANTRA
Mwili mzima, roho yenye mwanga,Nimejazwa na mwanga wa uponyaji.×7