✨ Siku mbili kabla ya Mwezi Mwandamo wa Kupatwa katika Pisces — Agosti 26, 2026
HUHITAJI KUWA MTU MWINGINE ✨ UNAKUMBUKA TU WEWE ULIYEKUWA KABLA MAISHA HAYAJAKUFUNDISHA KUJIFICHA
Huenda uponyaji haujawahi kuwa kuhusu kujibadilisha na kuwa mtu mwingine kabisa.
Labda uponyaji wa kweli unatokea pale tunapoanza kuachilia hofu tulizojikusanyia, majukumu tuliyojifunza kuyabeba, matarajio tuliyorithi na kinga tulizojijengea ili kujilinda.Chini ya yote hayo, kuna wewe halisi ambaye amekuwa akisubiri kuonekana. Si mtu mpya bali ni toleo lako la kweli ambalo lilifichwa na mambo ambayo maisha yalikufundisha kuyabeba.Leo Mwezi unaendelea kupitia Pisces, ukituelekeza kuelekea Ijumaa, wakati kutakuwa na Mwezi Mwandamo wa Kupatwa (Lunar Eclipse). Zimesalia siku mbili tu, na unaweza kuanza kuhisi uzito wa kihisia wa kipindi hiki.
Pisces ni alama ya mwisho katika zodiac, inayohusishwa na kukamilika, kujisalimisha, huruma, intuition na kuachilia mipaka ya zamani. Kwa hiyo, ni mahali panapofaa kwa eclipse inayofunga kipindi ambacho kimekuwa kikitufanya tujiulize ni mambo gani bado yana nafasi katika maisha tunayojenga.🌑 Kivuli hakimaanishi mwanga wako umeondokaKisayansi, wakati wa Lunar Eclipse, Dunia hupita kati ya Jua na Mwezi, na kivuli cha Dunia huangukia kwenye uso wa Mwezi.Tunaweza kulitumia hili kama mfano wa safari yetu ya ndani: nini hutokea mwanga wetu unapokutana na vivuli tulivyokusanya ndani yetu?Si lazima tupigane na vivuli hivyo. Wakati mwingine tunahitaji tu kuviona ili kuelewa kile ambacho vimekuwa vikificha.
Mambo mengi tunayobeba leo yaliwahi kuwa na sababu.Moyo uliojifunza kujilinda huenda ulikuwa na sababu ya kufanya hivyo.Mtu aliyezoea kuwajibika kwa kila kitu huenda aliwahi kulazimika kushikilia kila kitu pamoja.
Na sauti iliyojifunza kunyamaza huenda ilijifunza kwamba kuonekana kikamilifu haikuwa salama wakati fulani.Kwa hiyo, uponyaji si kujihukumu kwa kuwa uliwahi kuwa hivyo.Unaweza kuziheshimu na kuzishukuru versions zako za zamani kwa kukufikisha ulipo leo lakini usiziruhusu ziamue ni umbali gani unaoruhusiwa kwenda kesho.
🌊 Ujumbe wa Pisces EclipseMaji hayahitaji kulazimishwa kurudi katika hali yake ya asili. Ukiondoa kitu kinachoyazuia, yanakumbuka namna ya kutiririka.Na huenda hivyo ndivyo inavyotokea ndani yako sasa.Chini ya miaka ya matarajio, maumivu, majukumu, kujibadilisha ili kuwafurahisha wengine na simulizi za zamani, asili yako halisi bado ipo.Mwanga wako haukupotea.
Uliwekewa tu tabaka juu yake.💫 Jiulize swali hiliTunapoingia katika siku mbili za mwisho kabla ya Pisces Lunar Eclipse, huenda si lazima ujiulize:“Ninapaswa kuwa nani sasa?”Badala yake, jiulize:“Ni kitu gani hatimaye niko tayari kuacha kujificha nacho?”Huenda huhitaji utambulisho mpya.Huenda huhitaji toleo jipya kabisa la wewe.Huenda huhitaji kuongeza mwanga zaidi.Huenda unahitaji tu kuondoa kile ambacho kimekuwa kikisimama kati yako na mwanga ambao tayari ulikuwa ndani yako.
✨💖WE ARE ONE ♡
Dr.Mwaka✍️