UTABIRI WA NAMBA — 15 AGOSTI 2026
NAMBA 1 — 1, 10, 19, 28
Leo ni siku nzuri ya kupanga mambo yako ya baadaye. Unaweza kuwa katika hali ya kujisikia huru na kutokuwa na mawazo mengi. Ni wakati mzuri kukamilisha ununuzi wa kiwanja au mali kama ulikuwa unapanga kufanya hivyo. Bahati nzuri inaweza kukujia. Pia kuna uwezekano wa kuvutiwa na mtu mwingine nje ya mahusiano yako, hivyo kuwa makini usifanye jambo ambalo baadaye utalijutia.
Namba ya bahati: 18
Rangi ya bahati: Saffron
NAMBA 2 — 2, 11, 20, 29
Marafiki na ndugu wa karibu wako tayari kukusaidia. Unaweza kujisikia vizuri kwenda kula nje leo. Kama umekuwa ukifikiria kununua nyumba, leo ni siku nzuri ya kulifikiria jambo hilo. Hata hivyo, matumizi yanaweza kuwa makubwa kuliko mapato au faida unayotarajia. Kwa upande wa mapenzi, ni siku nzuri kumuonyesha mwenza wako kwamba uko serious na uhusiano wenu.
Namba ya bahati: 8
Rangi ya bahati: Nyeupe
NAMBA 3 — 3, 12, 21, 30
Kuna uwezekano wa kutokuelewana au ushindani kati yako na ndugu. Ni vizuri kuepuka mabishano na kuweka amani. Mama yako anaweza kuhitaji msaada wako leo. Kuwa makini kwa sababu unaweza kupoteza kitu cha thamani. Matumizi yanaweza kuongezeka na kukulazimisha kutumia baadhi ya akiba yako. Kwa upande wa mapenzi, hisia za kimapenzi zinaweza kuwa kali zaidi na wewe au mwenza wako anaweza kutamani uhusiano wa karibu na wenye maana zaidi.
Namba ya bahati: 9
Rangi ya bahati: Rose
NAMBA 4 — 4, 13, 22, 31
Leo unaonekana kuwa katika nafasi yenye nguvu na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi. Kununua vitu vya nyumbani kunaweza kukupa furaha. Pia unajisikia vizuri kimwili, hivyo ni wakati mzuri kuanza mazoezi au mpango mpya wa afya. Kuna uwezekano wa kupata faida kupitia watu au biashara za nje ya nchi. Kwenye uhusiano, kama umekuwa ukiepuka kumkabili mwenza wako kuhusu jambo fulani, huenda ukahitaji kuwa wazi zaidi na kusimamia msimamo wako.
Namba ya bahati: 1
Rangi ya bahati: Maroon
NAMBA 5 — 5, 14, 23
Mtu mwenye mamlaka au mkubwa kazini anaweza kusaidia kuimarisha nafasi yako ya kazi. Pia unaweza kupata nafasi ya kujifunza au kupata maarifa ambayo umekuwa ukitafuta. Afya inaweza kuwa si nzuri sana leo, hivyo pumzika na usijichoshe. Kwenye biashara, unaweza kuhitaji kujaribu njia mbalimbali mpaka upate mkakati unaofanya kazi vizuri. Kwa upande wa familia na mapenzi, wewe na mwenza wako mnaweza kupata muda mzuri wa kufanya mambo ya kufurahisha pamoja.
Namba ya bahati: 15
Rangi ya bahati: Dark Green
NAMBA 6 — 6, 15, 24
Kuna uwezekano wa kuwa na jambo linalomhusu baba yako na afya yake, hivyo ni vizuri kumjali. Kushiriki katika shughuli za kikundi kunaweza kuwa na umuhimu leo. Kuwa mwangalifu kwa sababu kuna mtu anaweza kujaribu kukudanganya au kukupotosha. Hakikisha unachunguza taarifa vizuri kabla ya kuamini. Matumizi ya nyumbani yanaweza kuongezeka, lakini kuna dalili za uwezekano wa mapato kuongezeka pia. Kwenye mapenzi, kunaweza kuwa na mtu au jambo linaloingilia uhusiano wako; ni wakati wa kuchukua hatua na kuweka mipaka.
Namba ya bahati: 7
Rangi ya bahati: Royal Blue
NAMBA 7 — 7, 16, 25
Jambo la kisheria ambalo limekuwa likichukua muda linaweza kuanza kukuchosha kiakili. Unaweza kujisikia vizuri baada ya kununua vitu vya nyumbani. Nguvu zako za kimwili na za ndani zitakusaidia kukabiliana na changamoto za kikazi. Kwenye mahusiano, mambo hayako vizuri sana kwa sasa, hivyo ni muhimu kudhibiti hasira na maneno kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Namba ya bahati: 6
Rangi ya bahati: Coffee
NAMBA 8 — 8, 17, 26
Hakikisha unathibitisha taarifa unazopokea kabla ya kuzitumia au kuzisambaza, ili kuepuka aibu au makosa yasiyo ya lazima. Mama yako anaweza kuhitaji msaada wako leo, hivyo kuwa karibu naye. Pia ni wakati mzuri kupata kitu ambacho umekuwa ukikitamani, ingawa huenda ukahitaji kufanya juhudi zaidi kupata pesa zake. Kwa upande wa mapenzi, kama umekutana hivi karibuni na mtu mpya, usikubali haraka sana; mchunguze kwanza.
Namba ya bahati: 4
Rangi ya bahati: Violet
NAMBA 9 — 9, 18, 27
Kuna uwezekano wa kutokea mabishano ya mara kwa mara nyumbani, hasa kutokana na hasira au temperament yako. Watoto wanaweza kuleta habari njema kutoka shuleni. Kuwa mwangalifu na usalama wako wa kimwili. Kibiashara, unaweza kuwa na hamu kubwa ya kuwashinda washindani wako. Hata hivyo, upande wa mahusiano unaonekana kuwa na changamoto, hivyo ni muhimu kutenga muda wa kurekebisha mambo na mwenza wako.
Namba ya bahati: 2
Rangi ya bahati: Indigo