READINGS ZA KILA NYOTA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MERCURY RETROGRADE.

NJIA INAANZA KUWA WAZI SASA NI WAKATI WA KUFANYA UAMUZI 30 JUNI, 2026

Wapendwa,Leo ndiyo siku ya mwisho ya mwezi Juni. Mwezi Mpevu wa Capricorn umeleta mwanga katika mioyo ya wengi ndani ya saa ishirini na nne zilizopita, na inawezekana pia umefunua jambo muhimu ndani yako. Wakati mwingine ufunuo huja kwa uwazi mkubwa, lakini mara nyingine huja kwa sauti ya ndani inayokualika kuendelea mbele hatua kwa hatua.Leo pia tunaingia katika mzunguko mpya wakati Jupiter inaingia katika nyota ya Simba (Leo). Nishati hii inatukumbusha kuwa maisha yanatualika kila siku kuwa toleo bora zaidi la sisi wenyewe. Kila hatua mpya huuliza swali moja muhimu: utaendelea kutembea njia uliyoizoea, au uko tayari kuitikia mwito wa kweli wa nafsi yako?Siyo kila fursa imekusudiwa iwe yako, na si kila mlango ulio wazi ni sehemu ya safari yako. Hekima ya ulimwengu hufungua milango sahihi kwa wakati sahihi. Wajibu wetu si kulazimisha maisha yaende kwa ratiba tunayoitaka, bali kuwa na utulivu wa kutosha kutambua milango inayofunguka pale mawazo, moyo na matendo yetu yanapokuwa katika maelewano.Siku zinazofuata baada ya Mwezi Mpevu huleta nafasi ya kipekee ya kutafakari. Mwanga tayari umeonyesha kile kilichopaswa kuonekana. Sasa ni wakati wa kutumia maarifa hayo katika maamuzi, matendo na maisha yako ya kila siku. Mabadiliko ya kweli hutokea pale unapochukua hatua kulingana na kile ulichojifunza.Kesho tunaingia mwezi mpya wa Julai, mwezi unaobeba nishati ya kutafakari, hekima ya ndani, intuition, ukuaji wa kiroho na kujitambua zaidi. Huu ni mwezi wa kusikiliza sauti ya ndani na kugundua kwamba majibu mengi uliyokuwa ukiyatafuta yamekuwa ndani yako muda wote.Ikiwa moyo wako unahisi kuwa sura mpya ya maisha yako inakaribia kuanza, usihisi lazima uone njia yote kabla ya kuanza kutembea. Mara nyingi kinachohitajika ni ujasiri wa kuchukua hatua moja ya kweli. Maisha huendelea kufunua njia kadri unavyoendelea mbele kwa imani.Mwishoni mwa mwezi huu, jitazame kwa upendo na utambue umbali uliokwisha kufika. Kila changamoto, kila furaha, kila somo na kila uzoefu umechangia kukufanya kuwa mtu uliyekuwa leo. Tunapoingia Julai, tunaingia tukiwa na matumaini mapya, hekima zaidi na imani kwamba kila jambo linaendelea kutokea kwa wakati wake sahihi.

NYOTA ZA ARDHI (EARTH SIGNS)Ng’ombe (Taurus) • Mashuke (Virgo) • Mbuzi (Capricorn)

Mercury Retrograde inaleta ukweli kuhusu watu waliokudharau au kudhani hutafika mbali. Kuna mtu aliyesema amemalizana na wewe, lakini kwa sasa anafuatilia kila hatua unayopiga kimya kimya.Pia kuna mambo ya zamani yanarudi tena maishani mwako. Hii haimaanishi wapenzi wa zamani pekee, bali pia fursa zilizopotea, fedha ulizokuwa unasubiri, madeni ambayo hukulipwa na mazungumzo yaliyokwisha bila kupata hitimisho. Unaweza kusikia kutoka kwa rafiki wa zamani, mfanyakazi mwenzako wa zamani au hata mtu ambaye uliwahi kuwa naye kwenye mahusiano.Kuna mtu aliyekudharau hapo awali sasa anatambua kuwa kutokuwepo kwako kumeacha pengo kubwa kuliko alivyodhani. Anatamani kuwasiliana nawe lakini ana hofu kwamba hutampa nafasi au utampuuza.Kwa upande wa fedha, kuwa makini sana na kila jambo. Malipo yaliyochelewa, fedha ulizosahau au marejesho ya pesa uliyokuwa unasubiri yanaweza kuachiliwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu. Pia unaweza kushangazwa na mtu anayekudai ghafla akakumbuka kukulipa.Usivunjike moyo ikiwa mipango yako itachelewa wiki hii. Kile kinachoonekana kama kikwazo kinaweza kuwa kinaelekeza njia yako kwenye fursa bora zaidi yenye kipato kizuri au utulivu wa muda mrefu.Pia kuna nyaraka muhimu kama mikataba, makubaliano au hati za kifedha zinazohitaji uzisome kwa makini kabla ya kufanya uamuzi. Usikimbilie kusaini au kukubali jambo bila kupitia kila kipengele.Mercury Retrograde pia inakufundisha kuacha kubeba matatizo ya watu wengine. Baadhi yenu mtaanza kuweka mipaka na kusema, “Tatua tatizo lako mwenyewe.” Uamuzi huo utaleta mabadiliko makubwa katika maisha yako.Pia kuna mtu aliyekata mawasiliano nawe bila maelezo atajaribu kurudi kana kwamba hakuna kilichotokea. Atashangaa kuona safari hii ni wewe ambaye hutompa majibu wala umakini aliokuwa ameuzoea.Kwa maelezo zaidi kuhusu athari za Mercury Retrograde kwenye nyota yako, Love Readings za siku hiyohiyo zinapatikana.

NYOTA ZA HEWA (AIR SIGNS)Mapacha (Gemini) • Mizani (Libra) • Ndoo (Aquarius)

Mercury Retrograde inaleta uwazi kwenye mambo ambayo kwa muda mrefu hayakuwa na majibu. Utaanza kuunganisha matukio na kugundua ukweli ambao hapo awali hukuweza kuuona. Kuna mtu ambaye amekuwa akikuambia ukweli wa nusu, lakini sasa vipande vilivyokuwa vinakosekana vitaanza kujitokeza.Pia kuna mtu aliyedhani siri yake haitawahi kufichuliwa. Hata hivyo, kipindi hiki kinaonyesha kuwa ukweli unaanza kujitokeza, na mambo yaliyokuwa yamefichwa kwa muda mrefu yataanza kufunuliwa.Wakati huohuo, kujiamini kwako kunawafanya baadhi ya watu wasiwe na amani. Huelezi tena kila hatua unayochukua, na jambo hilo linawachanganya wale waliokuwa wananufaika na hali yako ya kutojiamini.Kuwa makini na maneno yako wiki hii. Ujumbe mmoja wa haraka unaweza kurekebisha jambo muhimu au ukamaliza uhusiano kabisa. Fikiria kwa makini kabla ya kutuma ujumbe au kujibu ukiwa na hasira.Mercury Retrograde pia inaleta nishati inayohusiana na soulmate. Kuna mtu kutoka maisha yako ya zamani anaweza kurudi kukutafuta. Hata hivyo, kurudi kwake kunaonekana zaidi kuwa kwa ajili ya kufunga ukurasa uliobaki wazi kuliko kuanzisha maisha mapya pamoja nawe. Anaweza kuwa rafiki wa zamani, mtu mliyewahi kuwa kwenye mahusiano au mtu ambaye hakukuonyesha msimamo wake. Anaweza kusema anataka kujua tu unaendeleaje, lakini lengo lake halisi ni kutafuta taarifa kuhusu maisha yako ya sasa.Baraka ya kipindi hiki ni kwamba mazungumzo ambayo karibu uyakwepe yanaweza kufungua mlango mkubwa wa mafanikio katika kazi, biashara au upande wa fedha.Kwa maelezo zaidi kuhusu athari za Mercury Retrograde kwenye nyota yako, Love Readings za siku hiyohiyo zinapatikana.

NYOTA ZA MOTO (FIRE SIGNS)Punda (Aries) • Simba (Leo) • Mshale (Sagittarius)

Mercury Retrograde inakufanya uwe mtu ambaye wengi hawawezi kuacha kumfuatilia. Kuna mtu anayejikuta akirudia kila mazungumzo aliyowahi kuwa nayo na wewe, akijiuliza alikosea wapi. Ingawa mbele za watu anaonyesha kana kwamba hajali, kwa siri anafuatilia maisha yako, anauliza habari zako kupitia watu wengine au anatumaini kuwa wewe ndiye utamtafuta kwanza.Hata hivyo, kipindi hiki kinakutaka uwe makini na maneno yako. Mambo madogo yanaweza kugeuka mabishano makubwa ikiwa kila mmoja atang’ang’ania kuwa yeye ndiye yuko sahihi. Chagua busara kuliko hasira.Pia jina lako linaendelea kutajwa katika mazungumzo ambayo hata hujui yanafanyika. Kuna mtu amekuwa akijaribu kushindana na wewe kwa siri, lakini ukweli unaanza kujitokeza. Huwezi kushindanishwa na mtu ambaye hana kiwango sawa na chako.Kwa upande wa kazi na maendeleo, kuna fursa iliyokuwa imekwama au jibu ambalo umekuwa ukilisubiri kwa muda mrefu linaanza kusonga mbele. Hata hivyo, litakuja kwa njia tofauti na ulivyokuwa umeitarajia. Usikate tamaa kwa sababu ya kuchelewa; kinachoonekana kama kikwazo kinaweza kuwa kinakupeleka kwenye nafasi bora zaidi.Mercury Retrograde pia inaweza kuleta hitilafu kwenye teknolojia au mipango ya kila siku. Simu, gari, GPS, miadi au vifaa vya mawasiliano vinaweza kukusumbua hasa unapokuwa na haraka. Punguza mwendo, hakikisha kila kitu kiko sawa kabla ya kuchukua hatua.Katika upande wa mapenzi, kuna mtu ambaye umekuwa ukijaribu kumsahau anaweza kurudi ghafla kupitia ujumbe, ndoto au mkutano usiotarajiwa. Inaonekana amerudi baada ya kugundua kwamba alichokuwa akikitafuta hakikuwa bora kuliko kile alichokiacha.Pia kuna mtu atanaswa kwenye uongo wake mwenyewe baada ya kusahau alimwambia nani taarifa gani. Maneno yake yataanza kujipinga, na ukweli utawekwa wazi bila wewe kufanya chochote.Kwa maelezo zaidi kuhusu athari za Mercury Retrograde kwenye nyota yako, Love Readings za siku hiyohiyo zinapatikana.

NYOTA ZA MAJI (WATER SIGNS)Kaa (Cancer) • Nge (Scorpio) • Samaki (Pisces)Mercury

Retrograde inaleta hisia zilizokuwa zimefichwa kwa muda mrefu. Kuna mtu anayemkumbuka yule mtu uliyekuwa zamani na anatamani angekuthamini kabla hujabadilika. Ingawa ameonekana kuwa baridi au mbali nawe, ukweli ni kwamba bado anakukumbuka zaidi kuliko anavyoweza kukiri. Kinachomzuia kukufuata ni kiburi.Kipindi hiki kinawalazimisha watu kukabiliana na matokeo ya maamuzi yao. Kuna mtu aliyedhani ungeendelea kumsubiri milele, lakini sasa anatambua kuwa uponyaji wako haukusimama ukimsubiri.Pia utaanza kupata uwazi wa kihisia. Hutakuwa tena ukifuatilia majibu au kulazimisha watu wakueleze walichokufanyia. Kinachokuwa muhimu kwako sasa ni amani ya moyo. Cha kushangaza ni kwamba ulipoamua kuachilia, ndipo majibu uliyokuwa ukiyatafuta yanaanza kujitokeza yenyewe.Intuition yako itakuwa kali sana kipindi hiki cha Mercury Retrograde. Unaweza kumfikiria mtu ghafla halafu akakupigia simu. Unaweza kuota jambo na baadaye likatokea. Zingatia ndoto zako, hisia zako za ndani na ishara unazoziona mara kwa mara, kwa sababu kuna ujumbe muhimu unaojaribu kukuongoza.Pia unaachilia hatia ambayo haikuwa yako tangu mwanzo. Kuna mtu aliyekufanya ujisikie kwamba makosa yake yalikuwa jukumu lako, lakini sasa unaanza kuona ukweli na kutambua namna ulivyokuwa ukidanganywa kihisia.Mazungumzo ya kifamilia yaliyokuwa yakiepukwa kwa muda mrefu yanaweza hatimaye kufanyika. Ingawa yanaweza kuanza kwa hali ya kutokuwa sawa, mwisho wake yana nafasi ya kuleta suluhisho na amani.Pia kuna mtu atafichua taarifa kwa bahati mbaya ambazo hakupaswa kuzijua. Hilo litadhihirisha kwamba amekuwa akifuatilia maisha yako kwa siri kwa muda mrefu.Vilevile, utagundua kuwa watu wawili wamekuwa wakizungumza kuhusu wewe kwa siri. Mmoja amekuwa akikutetea na kusimama upande wako, huku mwingine akijaribu kukuharibia sifa. Mwishowe ukweli utawekwa wazi na utajua ni nani anayekutakia mema na ni nani ambaye si mwaminifu kwako.Kwa maelezo zaidi kuhusu athari za Mercury Retrograde kwenye nyota yako, Love Readings za siku hiyohiyo zinapatikana.

NAWATAKIA MWEZI MPYA,ULIOJAA MWANGA MPYA, USTAWI NA MAFANIKIO.

8 thoughts on “READINGS ZA KILA NYOTA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MERCURY RETROGRADE.”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top