🦂 VENUS RETROGRADE + MERCURY KATIKA SCORPIO — 6 OKTOBA 2026Tarehe 6 Oktoba 2026,
Venus akiwa kwenye mwendo wa kurudi nyuma (Venus Retrograde) ataungana na Mercury katika ishara ya Scorpio, na kuleta nguvu ya ufafanuzi, ukweli na mambo yaliyokuwa yamefichika kujitokeza.
Scorpio inahusishwa na kuchunguza mambo kwa kina. Kwa hiyo, siku hii inaweza kukusukuma kuangalia zaidi ya kile kinachoonekana juu juu na kugundua ukweli ambao unaweza kubadilisha mwelekeo wa maisha yako.
Mercury anawakilisha fikra, akili, mawasiliano na namna tunavyofikiri, wakati Venus inahusishwa na mapenzi, mahusiano, uzuri, thamani na fedha.Kwa hiyo, kuna uwezekano wa kupata ufafanuzi muhimu kuhusu moja au zaidi ya maeneo haya:❤️ Mahusiano na mapenzi💰 Fedha na namna unavyopata kipato🧠 Namna unavyofikiri na kufanya maamuzi
✨ Thamani yako binafsi na namna unavyojioneshaJambo ambalo limekuwa likikuchanganya linaweza kuanza kupata majibu. Mazungumzo ya zamani yanaweza kurudi, ukweli unaweza kusemwa, au unaweza ghafla kuelewa kitu ambacho hukuweza kukiona hapo awali.
🦂 Kwa wenye placements za Scorpio, hii inaweza kuwa kipindi muhimu cha kuanza ukurasa mpya katika namna unavyofikiria kuhusu mahusiano, namna unavyotengeneza kipato, na hata namna unavyojionesha kwa ulimwengu.
✨ Ujumbe wa Oktoba 6:Usiogope ukweli unaojitokeza. Wakati mwingine ukweli hauji kuvunja maisha yako; unakuja kukuonyesha njia sahihi ya kuendelea.