You Are Not Lazy,Inconsistent Just Be Real! Life Happened!

✨ Baadhi yenu mnaendelea kuangalia mahali mlipodhani mngekuwa kufikia sasa, halafu mnajiita wavivu, watu wasio na msimamo, mlio nyuma, wasio na hamasa, au mlio poteza mwelekeo.Lakini ukweli ni huu.

Maisha yalitokea.Kitu fulani kiliingilia ile version ya mpango mliokuwa mmejiwekea mwanzoni.Kupoteza mtu.Kuhama.Kuachana.Tatizo la familia.Msukosuko wa kifedha.Hofu kuhusu afya.Hali ambayo ulilazimika kwanza kuipigania ili uinusuru nafsi yako, kabla hata hujaweza kufikiria kuhusu “kuwa productive” tena…Na sasa unajaribu kujijenga upya huku ukijihukumu kwa sababu husongi kwa kasi ileile uliyokuwa unasonga nayo kabla kila kitu hakijabadilika.

Hiyo si haki kwako!Wakati mwingine kitu kinachoonekana kama kurudi nyuma kumbe ni maisha yanakulazimisha usiendelee kujenga juu ya kitu ambacho tayari kilikuwa kinaanza kupasuka.Wakati mwingine kusimama kidogo kunafichua kile ambacho hakikuwa endelevu!Nani hakuwa kweli upande wako.Kitu gani hakikuwa na maana kifedha.Nini kilikuwa kinakumaliza nguvu.Kitu gani ulikuwa unakilazimisha.Kile ambacho tayari ulikuwa umekikua, lakini ulikuwa bize sana kukubali ukweli huo.Na hapana… si kila kikwazo kinachotokea ni lazima kiwe “muda wa Mungu uliopangwa.”Baadhi ya mambo yanauma tu.Baadhi ya mambo hayakuwa ya haki.Baadhi ya mambo usingeyachagua KAMWE.

Lakini mwelekeo mpya bado unaweza kutoka ndani ya jambo lililokuumiza.Swali sasa linakuwa…“Kipindi hiki cha maisha yangu kinaniomba nijenge nini kwa namna tofauti?”Sio kwa kasi zaidi.Sio kwa uzuri zaidi.Sio ili kila mtu akuone kwamba “umerudi tena.”Bali kwa namna tofauti.Kwa mipaka bora.Kwa utambuzi bora.Kwa mapumziko zaidi.Kwa mipango na mikakati zaidi.Kwa kujithibitisha kidogo.Kwa kupunguza presha ya kurudi kuwa yule mtu wa zamani.Hujaanzia sifuri. Unaanzia kwenye uzoefu.Kwa hiyo kama maisha yako yanaonekana kuwa kimya kwa sasa…Kama maendeleo yako bado hayaonekani wazi…Kama unaweka vipande vya maisha yako pamoja kwa faragha…Haimaanishi kwamba umefeli.Huenda tu unajenga upya kitu ambacho safari hii kina nafasi ya kudumu kweli.

🤍Mshirikishe mtu anayejijenga upya kimya kimya.

Hauko peke yako katika safari hii. 🤞🏽🤞🏽

Usomaji wa siku hiyo hiyo unapatikana 🔮✨

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top