Love Oracle Readings

💨 AIR SIGNS ❤︎♊ Gemini • ♎ Libra • ♒ Acquarius

Nyota za Hewa, kuna mtu ambaye ana hisia za kweli kwako. Anaweza kuwa ni Gemini au mmoja wa Nyota za Maji (Cancer, Scorpio au Pisces). Reading inaonyesha kuwa moyo wako unaanza kufunguka kwa uwezekano mpya.Hii inaweza kuhusiana na mapenzi, urafiki, familia au hata namna unavyojiona wewe mwenyewe. Spirit inakuhimiza kuongozwa na ukweli, uwazi na ukomavu wa kihisia.Kuna uwezekano mtu akawasiliana nawe kukuomba msamaha, kufanya mazungumzo ya kutoka moyoni au kukuletea ombi au fursa ambayo hukuitegemea. Kwa baadhi yenu, kipindi hiki ni cha kupata ujasiri wa kueleza hisia ambazo umekuwa ukizificha kwa muda mrefu.Mahusiano ndiyo yatakuwa eneo muhimu zaidi kwa sasa. Spirit inakukumbusha kuzingatia watu ambao kwa kweli wanakujali, wanakuunga mkono na wanawekeza upendo katika maisha yako. Acha kutumia nguvu zako nyingi kwenye mahusiano yanayokufanya uendelee kujiuliza una nafasi gani kwa mtu huyo.Mahusiano yenye afya yanapaswa kukuletea amani, si kukuweka kwenye hali ya kuchanganyikiwa kila wakati.Baadhi yenu pia mnafika katika hatua muhimu ya kufanya uamuzi. Ni wakati wa kuruhusu moyo na akili vifanye kazi pamoja. Usiruhusu hofu ndiyo ikufanyie maamuzi.Sikiliza sauti yako ya ndani (intuition), lakini pia kuwa mkweli kuhusu kile kinachoendana na maisha unayotaka kujenga siku zijazo.🪬

🌱 EARTH SIGNS ❤︎♉ Taurus • ♍ Virgo • ♑ Capricorn

Nyota za Ardhi, kwa sasa unaweza kuwa katika kipindi cha kupona, kujijenga upya au kujikita zaidi kwenye malengo na majukumu yako. Pia kuna uwezekano kwamba Aquarius au Gemini yuko kwenye nishati yako kwa kiwango kikubwa. Huenda kuna jambo unaloliombea au kulitarajia kwa matumaini makubwa.Spirit inaonyesha kwamba matumaini yanaanza kurudi moyoni mwako. Ikiwa umekuwa ukihisi kukata tamaa, kujiuliza kama upo kwenye njia sahihi au kama juhudi zako zimekuwa na maana, ujumbe huu unakukumbusha kuwa hauko nyuma kama unavyofikiri. Mambo yanaanza kujipanga kwa faida yako, lakini hatua ya kwanza ni kuamini tena kwamba kila unachotamani kinawezekana.Hiki ni kipindi chenye nguvu cha kuvutia (manifestation). Kile unachoweka nguvu zako kila siku kina nafasi kubwa ya kukua. Hivyo, kuwa makini na mawazo yako, maneno unayojisemesha na simulizi unalojijengea kuhusu maisha yako. Ikiwa umekuwa ukizungumza kwa mtazamo wa kukosa au kukatishwa tamaa, sasa ni wakati wa kubadili mtazamo na kuelekeza akili yako kwenye maisha unayotaka kujenga, badala ya kuogopa kupoteza yale uliyonayo.Pia huu ni wakati mzuri wa kuwekeza ndani yako mwenyewe. Jifunze ujuzi mpya, anza wazo la biashara ambalo umekuwa ukiliwaza, omba nafasi unayoitamani au chukua hatua ambayo umekuwa ukiiahirisha kwa muda mrefu.Spirit inakukumbusha kwamba tayari una kila unachohitaji ili kuanza. Usisubiri mpaka kila kitu kiwe kamili ndipo uchukue hatua.Baadhi yenu sasa mnaanza kutambua uwezo mkubwa mlionao. Kujiamini unakokutafuta hakutatokana na kuthibitishwa na watu wengine, bali kutatokana na wewe mwenyewe kutambua nguvu na uwezo ulionao.Amini vipawa vyako, amini maono yako, na usiogope kuwa kiongozi wa maisha yako mwenyewe.

🔥 FIRE SIGNS ❤︎♈ Aries • ♌ Leo • ♐ Sagittarius

Nyota za Moto, kuna mtu anataka kukuomba msamaha au ana jambo muhimu analotaka kukuambia. Anaweza kuwa ni mtu ambaye ulimzuia (blocked) au ambaye kwa sasa hamzungumzi kama zamani. Kwa baadhi yenu, badala ya mtu wa zamani, kuna mtu mpya ambaye anataka kuupeleka uhusiano wenu kwenye hatua inayofuata.Spirit inaonyesha kuwa unaingia katika kipindi ambacho juhudi zako za taratibu na za kudumu zitaanza kuzaa matunda. Huenda mambo yamekuwa yakisonga polepole kuliko ulivyotarajia, lakini usichukulie mwendo wa polepole kama kutokuwepo kwa maendeleo. Kila hatua unayochukua imekuwa ikijenga msingi imara wa mafanikio yako, na uko karibu zaidi na mwanzo mpya kuliko unavyofikiria.Pia kuna nishati mpya ya hamasa inarudi kwenye maisha yako. Inaweza kuwa ni fursa mpya, uhusiano mpya, wazo la biashara au ubunifu, au kurudi kwa motisha ambayo ilikuwa imepungua. Jambo hili litakurejeshea kujiamini na kukukumbusha sababu iliyokufanya uanze safari yako.Spirit pia inakushauri usiharakishe mambo. Si lazima kila kitu kitokee mara moja. Endelea kujitokeza, kuwa na nidhamu na kuendelea kufanya juhudi zako kwa uthabiti, kwa sababu ndizo zitakazokuletea mafanikio ya muda mrefu.Mwisho, kuna uwezekano mtu akakuletea ofa, mwaliko au fursa yenye uwezo wa kukua na kuwa jambo kubwa na lenye manufaa ikiwa utaipa nafasi.

🌊 WATER SIGNS ❤︎♋ Cancer • ♏ Scorpio • ♓ Pisces

Nyota za Maji, inaonekana kuna uamuzi muhimu unaohitaji kuufanya. Pia unaweza kuwa unahisi umekwama au unatamani kufanya jambo fulani, lakini wakati huohuo unahitaji kusimamia msimamo wako na kutimiza ulichokisema. Hali hii inaweza kukufanya ujisikie kama unavutwa pande mbili tofauti. Moyoni unaweza kusema, “Ninatamani kufanya hivi…” lakini pia unajua unapaswa kubaki mwaminifu kwa maamuzi na mipaka uliyojiwekea.Kwa sasa, akili yako imekuwa ikifanya kazi kupita kiasi. Baadhi yenu mmekuwa mkifikiria sana kuhusu hali fulani, mkirudia mazungumzo yaliyopita, mkihofia yatakayotokea baadaye au mkibeba mzigo ambao hakuna anayejua isipokuwa wewe mwenyewe.Unaweza kuhisi umekwama, lakini Spirit inaonyesha kwamba kinachokuzuia mara nyingi si mazingira yako, bali ni hofu, kujitilia shaka au kusubiri kitu kibadilike kwanza ndipo nawe uchukue hatua.Habari njema ni kwamba polepole unaanza kurudi kwenye nguvu zako. Spirit inakukumbusha kuwa una uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yako kuliko unavyoamini.Ni wakati wa kuacha kuruhusu wasiwasi uamue kwa niaba yako. Weka mipaka, panga mambo yako vizuri na shughulikia kila jambo hatua kwa hatua badala ya kujaribu kubeba kila kitu kwa wakati mmoja.Pia kuna uwezekano wa kushughulika na mtu mwenye tabia ya kutaka kutawala au kuamua kila kitu. Badala ya kuogopeshwa na nishati yake, simama imara kwenye msimamo wako.Huhitaji kubishana wala kujitetea kila wakati. Matendo yako, uthabiti wako na msimamo wako vitazungumza kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno.

🪬 Ikiwa ujumbe huu unaendana na hali yako, Love Readings za siku hiyohiyo zinapatikana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top